China imeutaka Umoja wa Ulaya uache mara moja kuorodhesha makampuni ya China katika vikwazo vyake dhidi ya Russia.
n
Wizara ya Biashara ya China jana ilisema licha ya mazungumzo ya mara kwa mara na juhudi za kushawishi, Umoja wa Ulaya haujabadilisha uamuzi wake, ukiorodhesha tena makampuni ya China katika kifurushi chake cha 19 cha vikwazo dhidi ya Russia, na kwa mara ya kwanza kuweka vikwazo dhidi ya viwanda vikubwa vya kusafisha mafuta vya China na wafanyabiashara wa mafuta, hatua ambazo zinapingwa vikali na China.
n
Wizara hiyo imesema China imekuwa ikipinga vikwazo vya upande mmoja ambavyo havina msingi wa kisheria kwa mujibu wa sheria za kimataifa au idhini ya Umoja wa Mataifa. Vitendo vya Umoja wa Ulaya vinakinzana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi wa China na Umoja huo, na kwamba vitadhoofisha sana ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa pande mbili, na kuathiri usalama wa nishati duniani.




