• Pakistan na Afghanistan zakubali kuendelea kusitisha vita  

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki tarehe 30 Oktoba ilitoa taarifa ya pamoja juu ya mazungumzo kati ya Afghanistan na Pakistan.

    n

    Taarifa hiyo imesema mazungumzo hayo yaliyopatanishwa na Uturuki na Qatar, yamehusisha pande nne ikiwa ni pamoja na Afghanistan, Pakistan, Uturuki na Qatar, na kufanyika kuanzia tarehe 25 hadi 30 Oktoba huko Istanbul, huku yakilenga kuhimiza utekelezaji wa makubaliano ya kusimamisha vita yaliyofikiwa kati ya Afghanistan na Pakistan tarehe 18 hadi 19 Oktoba huko Doha.

    n

    Kwa mujibu wa taarifa, pande zote zimekubali kuendelea kudumisha usitishwaji vita, na zitafanya mkutano wa ngazi ya juu tarehe 6 Novemba huko Istanbul, ili kuendelea kujadili na kuamua taratibu za kiutendaji juu ya utekelezaji wa usitishwaji vita.

    原文连接

    搜索