• Rubani apongezwa baada ya kufanikisha kutua kwa dharura ndege yenye hitilafu ikiwa na abiria 55

    Shirika moja la ndege nchini Somalia limempongeza mmoja wa marubani wake baada ya kufanikisha ndege yake ya abiria kutua kwa dharura kutokana na hitilafu ya kiufundi, kwenye pwani karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mogadishu, huku abiria wote 55 waliokuwa kwenye ndege hiyo wakinusurika.

    n

    Shirika hilo la ndege limesema uamuzi wa haraka wa rubani huyo ulikuwa muhimu katika kuwaokoa abiria 50 na wafanyakazi watano.

    n

    Wafanyakazi wa ndege hiyo aina ya Fokker 50, waliripoti tatizo muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Mogadishu asubuhi ya Jumanne na kuomba ndege irudi uwanjani. Ndege hiyo ilitua kwa mafanikio kwenye uwanja wa ndege, lakini haiwezi kusimama kwenye njia ya kutua na kuishia kwenye maji ya kina kifupi.

    n

    Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Ndege ya Somalia Bw. Ahmed Macalin Hassan amesema bado haijulikani kulikuwa na tatizo gani.

    n

    n

    原文连接

    搜索