• Zimbabwe yasitisha mazungumzo na Marekani kuhusu mpango wa ufadhili wa afya

    Gazeti la serikali la The Herald liliripoti Jumatano kuwa Zimbabwe imesitisha mazungumzo na Marekani kuhusu pendekezo la ufadhili wa afya.

    n

    Kwa mujibu wa ripoti hiyo, makubaliano yaliyopendekezwa yalitoa ufadhili mkubwa wa afya na badala yake Zimbabwe itoe idhini ya ufikiaji kamili wa data nyeti za afya za nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na sampuli za vimelea na taarifa za magonjwa kutoka kwa raia wake.

    n

    Katika chapisho kwenye mtandao wa X, msemaji wa serikali ya Zimbabwe Nick Mangwana alisema, tatizo lilikuwa kwamba Zimbabwe iliombwa kutoa rasilimali na data za kibaolojia kwa muda mrefu, bila dhamana ya upatikanaji wa chanjo au matibabu vinavyotokana na raslimali hizo. Marekani haikutoa ushirikiano wowote wa data zake za magonjwa na mamlaka za afya za Zimbabwe. Ripoti hiyo iliongeza kuwa kimsingi mpango huo haukuwa wa ulinganifu.

    n

    Ubalozi wa Marekani nchini Zimbabwe Jumatano ulitoa taarifa ukisema Marekani haijafurahishwa na uamuzi wa serikali ya Zimbabwe.

    原文连接

    搜索