n
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lin Jian amesema kufuatia mwaliko wa vmakamu wa raia wa Kenya, Afrika Kusini na Shelisheli, Makamu wa Rais wa China Bw. Hang Zeng, atafanya ziara katika nchi hizo kuanzia tarehe 22 hadi 30 mwezi
n
Bw. Lin amesema China na Kenya zimejenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya, China na Afrika Kusini ni washirika wa kimkakati wa kina katika zama mpya, China na Shelisheli ni washirika wa kimkakati.
n
Amesema katika miaka ya hivi karibuni, hasa tangu Mkutano Mkuu wa Beijing wa baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2024 ulipofanyika, chini ya miongozo ya kimkakati ya Rais Xi Jinping na viongozi wa Kenya, Afrika Kusini na Seychelles, uhusiano wa China na nchi hizo tatu umepata maendeleo makubwa. Kuaminiana kisiasa kumeimarishwa, ushirikiano wa kivitendo umezaa matokeo chanya katika nyanja mbalimbali, mawasiliano ya kiutamaduni kati ya watu kwa watu yameimarishwa, na mawasiliano na uratibu katika masuala ya kikanda na kimataifa pia vimeimarishwa.



