Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Pekka Haavisto ametoa wito kwa pande zinazohusika katika mapigano nchini Sudan kutumia majadiliano na kuondoa mvutano kama hatua muhimu kuelekea kusitisha mapigano kwa pande zote.
n
Taarifa iliyotolewa na Baraza Huru la Mpito la Sudan hapo jana imesema, alipokutana na wanahabari baada ya mazungumzo na viongozi wa ngazi ya juu wa Sudan, Haaviko amesema ni muhimu kuendelea kushiriki njia zinazotoa kipaumbele kwa ulinzi wa raia na kutafiti hatua za ujenzi wa uaminifu ambao unaweza kusaidia kuweka mazingira chanya ya mchakato wa kuaminika.
n
Ameongeza kuwa, Umoja wa Mataifa unashirikiana na wadau wote husika kumaliza mapigano nchini Sudan na kufungua njia kuelekea amani ya kudumu itakayopatikana kupitia majadiliano ya dhati na jumuishi.
n



