• Watu 9 wafariki katika ajali ya meli pwani ya Djibouti  

    Shirika la Kimataifa la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM) limesema, wahamiaji 9 wamefariki, na wengine 45 hawajulikani walipo kati ya abiria 320 baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka usiku wa kuamkia jumanne wiki hii katika pwani ya Djibouti.

    n

    Mpaka sasa miili ya wanawake watatu na wanaume sita imepatikana, huku zaidi ya watu 120 waliookolewa, wote raia wa Ethiopia, wakipata msaada katika Kituo cha Mwitikio wa Wahamiaji cha IOM kilichoko mjini Obock.

    n

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika hilo, wahamiaji wao walikuwa wanajaribu kuvuka Ushoroba wa Bab el-Mandeb kutoka Djibouti kwenda Yemen wakati ajali hiyo ilipotokea.

    原文连接

    搜索