Wizara ya Mazingira na Mpito wa Kiikolojia ya Cote d’Ivoire imetoa taarifa Jumamosi ikitangaza kuwa mji wa Abidjan umechaguliwa kuwa mwenyeji wa ofisi ya Mfuko wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (GCF) kanda ya Afrika.
n
n
Uteuzi huo ulitolewa kufuatia mkutano wa mfuko huo uliofanyika tangu Jumatano hadi JUmamosi wiki iliyopita huko Incheon nchini Korea Kusini.
n
n
Mamlaka nchini Cote d’Ivoire zimesema uamuzi huo unaakisi mwelekeo mzuri wa kiuchumi wa nchi hiyo na ahadi yake katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ukiichukulia Cote d’Ivoire kama mtendaji mkuu kwenye juhudi za Afrika za kukabiliana na suala hilo.
n
n
Kupitia uwepo wa kimkakati wa mfuko huo mjini Abidjan, GCF inalenga kuimarisha uratibu wa miradi yake, kuongeza uungaji mkono wa kiufundi kwa nchi mbalimbali, na kurahisisha upatikanaji wa ufadhili wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
n
n
n



