Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Bw. Mohammad Ishaq Dar amesema, Marekani na Iran zimeonyesha imani kwa Pakistan kuongoza mchakato wa mazungumzo, akielezea hatua hiyo kuwa ni maendeleo chanya katika mgogoro wa kikanda unaoendelea.
n
Akizungumza na wanahabari hapo jana baada ya mkutano wa pande nne uliofanyika mjini Islamabad, Bw. Dar amesema Pakistan imefurahia uaminifu ulioonyeshwa na pande hizo mbili, akiongeza kuwa amewafahamisha mawaziri na wajumbe kutoka Saudi Arabia, Misri na Uturuki kuhusu uwezekano wa mazungumzo kati ya Marekani na Iran kufanyika katika mji mkuu wa Pakistan.
n
Amesema Pakistan iko tayari kuandaa na kuwezesha mazungumzo ya kina kati ya pande hizo mbili katika siku zijazo, kwa ajili ya suluhisho la kudumu la mgogoro unaoendelea katika kanda ya Mashariki ya Kati.
n



